Wednesday, January 7, 2009

Mahakama imuamue Mkapa


Benjamin Mkapa, rais wa zamani wa Tanzania anaendelea kusakamwa na tuhuma lukuki za ufisadi. Tayari baadhi ya watu wakiwamo baadhi ya wanasiasa uchwara wanataka Mkapa aachwe kama alivyo.

Mkapa anatuhumiwa kutumia vibaya madaraka, kujilimbikizia mali na kufanya biashara akiwa Ikulu. Je, ni kweli kuna haja ya kuendelea kuhubiri kwamba Mkapa anatakiwa kuachwa kufanya atakayo?

Tuesday, December 30, 2008

Buriani Zeyana Seif




Zeyana Seif alikuwa mmoja wa watangazaji wa kwanza wa kike katika Idhaa ya Kiswahiri ya Radio BBC-Uingereza. Hapa ilikuwa mwaka 1959.

Baada ya albino, nani?


KATIKA Tanzania , baadhi ya wananchi wanawinda wananchi wenzao wenye ulemavu wa ngozi – Albino – na kuwaua.

Mauaji yanaenda sambamba na uvumi kwamba viungo vya albino ni mali na kwamba aliyenavyo aweza kupewa dawa ya kumwezesha kuwa tajiri.


Hivi sasa mbio za kupata utajiri zimechukua kasi ileile ya mauaji. Wengi wanatamani utajiri wa miujiza. Kadri fikra hizo zinavyozingatiwa, ndivyo albino wanavyoendelea kuangamia.

Sasa swali la kujiuliza: Baada ya Albino kuteketea kama msitu mkavu, nani wengine watakaofuata? Bila shaka, tusubiri muda si mrefu tutaona!

Monday, December 29, 2008

Pole Mayala

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PPR, Pascal Maya akiwa amelazwa katika Hospitari ya Apollo Indraprastha, mjini Delih nchini India anakotibiwa baada ya kujeruhiwa vibaya katika ajali ya pikipiki iliyotokea hivi karibuni nchini


Jana nilikwenda kumjulia hali mshikadau mwenzangu, Pascal Mayala aliyelazwa katika Hospitari ya Apollo Indraprastha, mjini Delih nchini India.

Mayala amelazwa hopitari hapo akipata matibu yaliotokana na ajali ya pikipiki miezi mitatu iliyopita nchini Tanzania ambapo alijeruhiwa vibaya mguu wa kushoto, mkono wa kushoto na bega la kushoto.

Sunday, December 28, 2008