Thursday, December 18, 2008

Serikali imechimbia kaburi kwa watoto wetu

Taarifa za hivi sasa zinasema, baada ya serikali kuamua kuwalipa malimbikizo ya posho zao, wanafunzi wanaosoma nje ya nchi kwa mpigo, ikiwamo posho ya chakula, nauli, ada na field, wanafunzi hao sasa wanazitumia fedha hizo kwa anasa. Hakika, wameamua kumwaga radhi mitaani.
Inaelezwa kwamba hali ni mbaya zaidi nchini India. Huko wanafunzi wa Kitanzania wanasema, “EPA imetuangukia. ” Wakati huu ambapo wanafunzi wamemaliza mitihani, wanafunzi hao wameweka makazi katika mji wa Mysore, ambapo watoto wa Kibongo wanashinda mbinu za kuchuna na wenzao wa Kagame.

Kuna uwezekano mkubwa kwa wanafunzi hao kushindwa kumaliza masomo, kutokana na kuzitumia fedha hizo vibaya. Wengi pia watarejea nyumbani wakiwa tayari wamebeba ukimwi. Wazazi jiandaeni kuwapokea. Lakini lawama zote mtupieni JK aliyeamua si tu, kuwalipa malimbikizo yao kwa mpigo, bali kusitisha malipo hayo tena.

No comments: