Wednesday, December 17, 2008

ATC iko ICU, Mataka anaendelea kuula

HAPA Mkurugenzi Mkuu wa ATC, Mataka anaonekana akishuka katika ndege ya kukodi ya ATC mapema mwaka huu, huku akijitapa kwamba shirika hilo litakuwa imara na lenye hadhi ya kimataifa kabla ya miaka 2 ya utawala wake. Lakini sasa ni dhahiri ndoto za Mataka zimeyayuka. ATC iko hoi kiuchumi. Tayari imesimamisha sfari zake nchi mzima. Lakini wakati hayo yakiendelea, pamoja na kushindwa kabisa kuokoa shirika bado anang'ang'ania ofisi.

No comments: