Thursday, December 18, 2008

Nape kujiunga Chadema?
Mwanasiasa kijana Nape Nnauye, anadaiwa kutaka kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Taarifa hizi tayari zimetinga Ikulu ya Kikwete na jana Jumatano wakubwa walikuwa wanahaha kuhakikisha Nape haondoki katika chama chao.

Inaelezwa kwamba hofu ya watawala ni kuwa iwapo Nape akijiunga na Chadema, CCM kinaweza kusambaratika kutokana na ukweli kwamba katika siku za karibuni, CCM kimekubwa na kashifa ya UFISADI na Nape anazijua siri zao katika kufanikisha ukwapuaji wa mabilioni ya wananchi.

Nape alinithibitishia leo kuwapo kwa taarifa hizo, ingawa aligoma kuingia kwa undani.

No comments: