Tuesday, December 30, 2008

Baada ya albino, nani?


KATIKA Tanzania , baadhi ya wananchi wanawinda wananchi wenzao wenye ulemavu wa ngozi – Albino – na kuwaua.

Mauaji yanaenda sambamba na uvumi kwamba viungo vya albino ni mali na kwamba aliyenavyo aweza kupewa dawa ya kumwezesha kuwa tajiri.


Hivi sasa mbio za kupata utajiri zimechukua kasi ileile ya mauaji. Wengi wanatamani utajiri wa miujiza. Kadri fikra hizo zinavyozingatiwa, ndivyo albino wanavyoendelea kuangamia.

Sasa swali la kujiuliza: Baada ya Albino kuteketea kama msitu mkavu, nani wengine watakaofuata? Bila shaka, tusubiri muda si mrefu tutaona!

1 comment:

Subi Nukta said...

Hakuna cha kusubiri kaka Kubenea,
Tumeshaona jinsi waongo wanavyowaimanisha watu kuwa viganja ya mikono vyenye alama fulani vinafaa kuleta utajiri.
Zamani waliwahi kusema watu wenye upara ndiyo wenye kufaa.
Alimradi binadamu hakosi sababu!
Inaudhi mno!