Friday, April 4, 2008

Huu ni ujuha wa mwingine

KAMPUNI ya Kupakua shehena nchini Tanzania International Container Terminal (TICTS), ambayo inamilikiwa na mwanasiasa aliyefukuzwa uwaziri na Bunge, Nazir Karamagi, inakwapua mabilioni ya shilingi kila mwaka, huku Watanzania wakiambulia patupu.

Wakati TICTS ikiwa imechota Sh. 172.3 Bilioni kwa mwaka wa fedha 2006/2007, serekali iliambulia kiasi cha Sh. 5 Bilioni. Hizi ni fedha ambazo hazitoshi hata kujenga matundu ya shule katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kwa ajili ya watoto waliofaulu kwa mwaka huu wa 2007.

TICTS inachota kiasi hicho cha fedha huku ikiwa haijaweka hata shilingi kwa ajili ya miundombinu badala yake imekuwa ikitumia miundombinu ya Bandari.

Aidha, Karamagi amedhihirisha kwa mara nyingine tena, kwamba ni bingwa wa kuingiza serikali mkengeni. Ni huyu ambaye amekili kusaini mkataba wa kinyonyaji wa Buzwagi mkoani Shinyanga na mkataba wa kufua umeme wa dharula kati Tanesco na kampuni ya Richmond na dada yake Dowans.

Je,

No comments: