Saturday, February 23, 2008

Ni Kweli Fisadi No 1 ameachia ngazi?


Jana Edward Lowassa, waziri mkuu aliyefukuzwa kazi kwa tuhuma za ufisadi, aliwasili mjini Arusha na kuthibitisha mambo mawili. Moja, kwamba yeye ni fisadi wa hali ya juu sana. Hili linathibitishwa na jinsi mapokezi yake yalivyokuwa.

Kwanza, yaliandaliwa na watuhumiwa wakuu wa ufisadi ukiwamo ujambazi kama Nyari. Pili, yaligharimu mamilioni ya fedha, hali inayothibitisha kwamba zile hazikuwa fedha zilizopatikana kupitia njia ya kawaida.


Mbili, mapokezi yake yanaonyesha kwamba Lowassa hajafa kisiasa, bali anajipanga upya ili ajitumbukize katika siasa siku zijazo.

6 comments:

Anonymous said...

ulifikiria ndugu yangu kuwa lowasa anaacha siasa?kumbka nyie magazeti ndo mnmpandisha chati,anaglia south africa sasa zuma anafanya nini,ndo rais ajae baada ya mbekhi,na kashifa zote,ndo siasa mkubwa magazeti yenyewe kila siku ni habari za lowasa,mi nadhani una kisa na lowasa coz hii bloggle inamjadilisana lowasa,haaaaa

Anonymous said...

NDUGU YANGU KUBENEA NAONA SASA UMEAMUA KUFANYA KAZI ZA TUME NA MAHAKAMA KWA PAMOJA. KAMA MAHAKAMA HAIJAHUKUMU WEWE UMEAMUA KUHUKUMU.....INSHAALAH.

Saed Kubenea said...

Kamati ilikosea, Kubenea ana haki ya kusema hilo. Huyo ni jambazi mkubwa. richmond ni yake. Hakuna ubishi na hawezi kutoka hapo, aende aendako.

Saed Kubenea said...

Kamati ilikosea, Kubenea ana haki ya kusema hilo. Huyo ni jambazi mkubwa. richmond ni yake. Hakuna ubishi na hawezi kutoka hapo, aende aendako.

Anonymous said...

Hivyo hivyo kaka kubenea kaza buti, tuko nyuma yako, ukweli lazima ujulikane katika hizi skendo, aluta continua, mapambano bado yanaendelea.

Anonymous said...

Huyu jamaa anayemtetea lowasa ni ndugu yake au vipi, Lowasa ni jambazi, hili halina ubishi. Kama si hivyo mbona alishindwa kujitetea ndani ya bunge. Ameenda kudeseshwa na washauri wake kuaanza kuwaruka wakina karamagi. Lazima awajibishwe tu.