Tuesday, January 29, 2008

Urais waigawa familia ya Karume



Na Jabir Idrissa

SASA ni dhahiri kwamba kuna mgawanyiko ndani ya familia ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar baada ya mapinduzi ya 12 Januari 1964.

Kitendo cha Balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Abeid Amani Karume (Balozi Karume) cha kujitokeza na kutangaza wazi kuwa anakusudia kuchukua fomu ya kuomba uteuzi ili agombee kiti cha rais wa Zanzibar mwaka 2010, kinaonyesha mgawanyiko mkubwa.

Balozi Karume ni mdogo wa rais wa sasa wa Zanzibar, Amani Abeid Karume. Hili haliwezi kuchukuliwa kuwa ni mgongano tu kati ya ndugu, bali mpasuko wa aina yake na wa kisiasa, katika Zanzibar na ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ni wazi sasa kuwa mwanasiasa balozi na rais wake, hawaivi katika chungu kimoja. Unafuu wa balozi ni kwamba anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano na siyo rais wa Zanzibar.

Kama vile hiyo haitoshi, kauli ya Balozi Karume, ya kutaka kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani, akisema ndio suluhisho la kipekee la kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa kisiasa Zanzibar, imeweka wazi zaidi tofauti kati ya ndugu hao wawili.

Balozi Karume ambaye amekuwepo nchini baada ya kuhudhuria mkutano maalum wa mabalozi wote 32 walioko nchi za nje uliofanyikia Unguja, ametoa matamko hayo mawili mazito mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Zanzibar.
MwanaHALISI Januari 30-Februari 5, 2008.

Je, wewe unasemaje?

1 comment:

Anonymous said...

sinahakika lakini nacho fahamu huyu Abeid Karume aliye madarakani hivi sasa anamaliza muda wake hapo 2010 na kwa katiba ya nchi yatu hawezi kugombea tena sasa sijui hapo mgawanyiko uko wapi hizi habari kabla ya kuandika hebu tuwe tunafanya utafiti jamani uandishi wa habari sio kama kutoa stori kijiweni.