Thursday, January 24, 2008

SERIKALI YAJIVUA NGUO



SASA imethibitika rasmi kwamba serikali ilichota dola za Kimarekani 30.7 milioni kupitia kampuni ya Kagoda Agriculture Limited (KAL), MwanaHALISI linaweza kuthibitisha.

ya Rais Jakaya Kikwete iliidhinisha na kuruhusu Benki Kuu ya Tanzania (BoT) itoe zaidi ya

Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, kwa mujibu wa kumbukumbu zilizoko Wakala wa Usajili wa Makampuni nchini (BRELA), inamilikiwa na Rostam Aziz, mfanyabiashara, mwanasiasa na mmoja wa watuhumiwa 11 wa ufisadi.

Taarifa za uhakika ambazo MwanaHALISI inazo, zinabainisha kuwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji ameyathibitisha malipo hayo kwa wakaguzi wa Deloitte & Touche wa Afrika Kusini waliofanya ukaguzi kwenye benki hiyo kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni, 2006.

Imegundulika kwamba Waziri Meghji aliwaandikia wakaguzi hao wanaopatikana kwa anuani No X6, Gallor Manor 2052, Johannesburg, akiwafahamisha kwamba malipo ya dola 30,732,658.82 kwa KAL kupitia BoT yaliidhinishwa na Serikali.

“Kama ujuavyo Serikali huru zinakuwa na siri na umuhimu wa kufanya malipo ya kugharamia shughuli zake kwa usiri mkubwa. Kwa sababu hiyo basi, na kwa namna suala hili tulivyojadiliana nawe.

“Malipo (hayo) yaliidhinishwa na Serikali na kutumika na Serikali kwa ajili ya kugharamia shughuli nyeti za Serikali,” amesema waziri huyo kwenye barua ya 15 Septemba, 2006 yenye kumb. MF/GEN/2006 aliyoisaini yeye mwenyewe.

Waziri Meghji amesema kwamba ametoa uthibitisho huo kwa sababu ni muhimu kuchukua hatua hiyo katika kuimarisha jukumu muhimu la kuendeleza usiri katika kazi za serikali.

Ndani ya barua hiyo, Waziri Meghji pia amesema kwamba hakuna malipo mengine yaliyoidhinishwa kutolewa na BoT katika kipindi cha kati ya 1 Julai, 2005 na 30 Juni, 2006.

“Kwa hakika, si jambo la kawaida hata kidogo Serikali kulazimika kujitokeza na kutoa taarifa za siri kama hizi na hutokea tu pale inapoona ipo haja ya kufanya hivyo kwa maslahi ya taifa,” amesema Waziri huyo katika barua hiyo ambayo haikuwekwa muhuri maalum unaotambulisha kuwa suala hilo ni “siri ya serikali.”

Amehitimisha barua kwa kusema: Ninapenda kuthibitisha kwamba hatua iliyochukuliwa na serikali katika mazingira haya imefuata mkondo wa sheria za nchi.

Uthibitisho huo unarudi nyuma kuonyesha kwamba Serikali yenyewe iliidhinisha malipo ya hujuma dhidi ya fedha za umma kwa kampuni binafsi ambayo mazingira ya kusajiliwa kwake yamejaa utata.

Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, ilitajwa hadharani kwa mara ya kwanza kuhusika na ufisadi na mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa (Chadema).

Dk. Slaa alituhumu kampuni ya akisema ilichota mabilioni hayo ya shilingi katika kipindi cha uchaguzi mkuu.



KAMPUNI binafsi iliyosajiliwa kwa anwani ya Dar es Salaam na kuchotewa shilingi bilioni 40/= baada ya muda mfupi haina ofisi mjini Dar es Salaam na anwani iliyoandikwa katika daftari la usajili ni ya udanganyifu.

Kampuni hiyo iitwayo Kagoda Agriculture Limited, ililipwa mabilioni hayo ya fedha za walipa kodi mwaka 2005. Pesa hizo zilikuwa katika Dola za Marekani milioni 30.8 ambazo thamani yake ni sawa na bilioni 40/=.

Uchunguzi wa THISDAY dada wa KULIKONI umebainisha kwamba anwani ilIyotajwa katika usajili wa kampuni hiyo - Kitalu namba 87 eneo la viwanda la Kipawa, Wilaya ya Temeke - ni ya uongo kwani hakuna kitalu kama hicho katika ramani kuu ya Jiji la Dar es Salaam.

Habari za uhakika za uchunguzi toka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, zinatuthibitishia kwamba hakuna kitalu kama hicho popote.

“Ninasikitika hatuna kitalu chenye namba hiyo kwenye orodha katikaa Ofisi ya Usajili wa Viwanja,” ofisa mwandamizi wa Wizara ya Ardhi alisema alipoombwa kusema kuhusu suala hilo.

Uchunguzi umethibitisha kwamba kampuni ya Kagoda haikuwahi kuwa na ofisi popote na kwamba hata Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) haikuwahi kupokea malipo yoyote ya kodi kutokana na malipo ya mabilioni ya biashara isiyoeleweka.

Cha ajabu zaidi katika usajili wa kampuni hiyo ni majina ya wanahisa waliosajili kampuni hiyo ambao hawafahamiki kabisa. Majina yao ni John Kyomuhendo (hisa 40) na Francis William (Rostam) ((hisa 60), ambao wote wana anwani moja (S. L. P. 80154, Dar es Salaam) na kutajwa kama wakazi wa Dar es Salaam.

Vyanzo vya habari vya kuaminika vimesema Kyomuhendo anafanya kazi na kampuni moja ya ujenzi maeneo ya Kipawa na anadhaniwa kutumia jina la udanganyifu kuficha utambulisho wake halisi.

Taarifa katika rekodi za Serikali zinaonesha kwamba Francis William alisajili kampuni ya Kagoda Septemba 29, 2005, na kupewa cheti cha usajili namba 54040. Shahidi wake katika usajili ametajwa kwa jina la Benjamin Mwangonda ambaye ni mhasibu wa kampuni iitwayo Khatco Management Limited.

Majukumu ya kampuni yanatajwa kuwa ni: “Kufanya biashara ya kilimo na ukulima wa aina mbalimbali ya mazao ya kilimo kwa ajili ya chakula au biashara, ufugaji na maziwa. Pia itazalisha kuku, bata, bata-mzinga, kutengeneza jibini, na mbogamboga za majani kwa ajili na kuuza nje ya nchi.

Kagoda Agriculture Limited imesajiliwa pia kwa ajili ya “kuuza nyama, mayai, kuku, vyakula vya kuku, madawa ya kuku, na vifaa vya kufugia kuku; kuuza nje maua; na kujenga nyumba mashambani vyumba vya kupoozesha na barabara.”

Imebainika katika ukaguzi wa kihasibu kwamba kampuni hiyo ilichotewa mabilioni ya fedha zikiwa katika dola kutoka Benki Kuu ikiwa ni mtiririko wa ufisadi kabambe ndani ya Benki Kuu.

Maofisa kadhaa waandamizi wa Benki Kuu wanatuhumiwa kushiriki katika njama hizo za ufisadi.

Kwa mujibu wa taarifa za wakaguzi wa hesabu wa kampuni ya Deloitte & Touche mwaka jana, ufisadi huo ulifanyika kwa mbinu kabambe za kughushi nyaraka mbalimbali Benki Kuu ambayo ni muhimu zaidi katika Sekta ya Fedha na Uchumi hapa Tanzania.

Kama ilivyokwishaandikwa katika matoleo ya awali ya KULIKONI na dada yake THISDAY, Kagoda Agriculture Limited, ililipwa na Benki Kuu fedha hizo (dola 30,732,658.82) kutekeleza majukumu 12 ya miradi ambayo haifahamiki vizuri lakini inayohusu “wafadhili”, “wahisani” au “wakopeshaji” muhimu wa Serikali.

Kampuni ya Deloitte & Touche, ambayo hadi mwaka jana ilikuwa ndio mkaguzi wa ndani wa hesabu za Benki Kuu inasadikiwa kuingia mgogoro kuhusu madeni na malipo ya Benki Kuu katika akaunti namba 99915091 01.

Wakati wa ukaguzi wa hesabu za kihasibu katika kipindi kilichoishia mwaka Juni 30, 2006, akaunti hii ilikuwa na fedha kiasi bilioni 131.95/-.

Kwa kufuatilia maneno yaliyo katika nyaraka ya kurasa nne kutoka Deloitte & Touche kwenda kwa Gavana wa Benki Kuu, Dk. Daudi Ballali, yenye tarehe Septemba 04, 2006, kuna maelezo yanayoonesha kasoro katika malipo ya fedha kwa Kagoda Agriculture Limited kama ifuatavyo:

• Kuna makubaliano 12 ya majukumu ya kutekelezwa kati ya Septemba 10, 2005 na Novemba 05, 2005. Muda huo hapo juu ni mfupi mno kwa kulipa wadai 12 mbalimbali dunia nzima.

• Makubaliano yote yalitiwa saini mjini Dar es Salaam mbele ya ofisa mmoja aitwaye B.M. Sanze, ambaye ni wakili wa Mahakama Kuu.

• Makubaliano matano yalifikiwa kwa kutiwa saini Oktoba 19, 2005 wakati makubaliano manne yaliwekwa saini Oktoba 18, 2005. Hii inaonesha kwamba wadai wa nje walisafiri na kuwahi kuweka saini zao katika makubaliano hayo katika muda wa siku moja. Uchunguzi katika Idara za Uhamiaji unaweza kubainisha kama jambo hili liliwezekana lakini akili za kawaida zinakataa uwezekano huo.

• Kuna makubaliano mawili ya majukumu yaliyofikiwa kwa saini Oktoba 18 (2005) yakihusu kampuni mbili za Kijerumani (Lindeteves J Export BV na Hoechst) kuhusu malipo ya Euro 1,164,402.76. Hata hivyo tarakimu zilikosewa na Benki Kuu ilindika barua kwa Kagoda Agriculture Limited kuelezeka kwamba malipo yatathiminiwe kwa fedha ya Kijerumani - Deutsche Marks. Barua hiyo hiyo ilishauri kutolewa kwa kiasi cha 8,196,673,600.53/- kwa Kagoda Agriculture Limited. Hatimaye wadai (Kagoda) waliwasilisha makubaliano mapya ya majukumu yenye tarehe Novemba 03, 2005 – siku mbili tu baada yta kuarifiwa.

• Tumebaini sio kawaida na tuna mashaka makubwa kwamba wadai wa fedha wa nje wanaweza kufanya makosa ya kujichanganya hadi kusahau na kuweka saini katika makubaliano yenye aina ya fedha tofauti na wanazostahili kulipwa (Euro badala ya Deutsche Marks). Juu ya hapo inaonesha udhaifu mkubwa kwa Benki Kuu kushindwa kufanya uchunguzi baada ya kubaini kasoro katika suala hilo. Badala yake Benki Kuu hiyo hiyo ikaendelea na mchakato wa kutoa malipo makubwa kiasi cha bilioni 8.2/- kwa wadai (kampuni tata ya Kagoda). Pia inashangaza ni vipi wakurugenzi wa Kagoda waliweza kurudi ghafla nchini katika kipindi cha siku mbili tu na kushughulikia marekebisho ya ghafla ya makubaliano. Hapo napo panahitaji uchunguzi katika Idara ya Uhamiaji kubaini safari za maofisa hao zilivyofanikishwa sambamba na matukio yaliyopo.

• Makubaliano yote 12 ya majukumu yanaonekana kuwa na lugha na maneno ya aina moja katika wadai wote wa kigeni. Hili sio jambo la kawaida kwani kampuni zisiohusiana haziwezi kutumia lugha inayofanana katika nyaraka zake.

• Hakuna makubaliano yoyote ya majukumu hayo 12 yaliyo katika karatasi zenye nembo za kampuni husika, hakuna anwani za kampuni husika au wawakilishi wake.

• Makubaliano yote yametiwa saini kurasa ya mwisho na wawakilishi wa wadai 12 wa dunia nzima. Hili sio jambo la kawaida kwani nyaraka za kisheria huwa zinakuwa na sahihi kila kurasa.

• Mihuri ya moto (seal) katika nyaraka zote 12 inaonesha kwamba inafanana na ya Kagoda Agriculture Limited. Uchunguzi umethibitisha kwamba watengenezaji wa mihuri yote 12 wanaweza kuwa “msanii” mmoja katika mbinu za kughushi.

• Kampuni tatu: Fiat Veicoli Industriali (kampuni ya Kitaliano), Valmet (Kampuni ya Marekani), na Adriano Gardella S.P.A (Kampuni ya Kitaliano ) zina mihuri ya moto inayofanana kabisa licha ya mikataba kuonesha kwamba zinatofautiana.

• Makubaliano ya Valmet, ambayo ni kampuni ya Marekani ni dola 2,398,439.96 lakini mkataba umesainiwa na Patrick Kevin, ambaye wadhifa wake katika kampuni hiyo ni “mhasibu.” Hii inashangaza kwamba makubaliano muhimu na ya gharama kubwa namna hiyo yatafikiwa na “mhasibu” katika kampuni.

• Mkataba wa Daimler Benz AG umesainiwa na mkurugenzi aitwaye Christopher Williams. Cha ajabu saini inaonesha herufi W. Christopher.

• Kampuni kadhaa zilizotia mkataba zilikwisha fungwa au kufutwa kama kampuni katika orodha ya usajili wa kampuni tarehe za zinazooneshwa katika mikataba. Hiyo ni kwa mujibu wa uchunguzi wa kampuni ya Deloitte & Touche.

• Kwa mfano, Hoechst AG ilishabadilishwa kuwa Aventis mwaka 1999. Daimler Benz AG nayo ilishabadilishwa kuwa Daimler Chrysler AG mwaka 1998. Fiat Veicoli Industriali halikadhalika ilishabadilishwa kuwa Industrial Vehicle Corporation (IVECO) January Mosi, 1975. Vilevile Mirrlees Blackstone iligeuzwa jina kuwa MAN B&W Diesel Limited kutoka Machi 2002, wakati Valmet ilibalidishwa kuwa Metso Paper toka Mei 10, 2000. Sasa inashangaza kabisa majina ya zamani ya makampuni haya kutumika katika mikataba inayohusu mamilioni ya fedha mwaka 2005.

• Hakuna majina ya kampuni zilizopatikana katika majedwali zinazoitwa NS Boma na Lindeteves J. Export BV.

• Simu zilizopigwa katika ofisi za makampuni yaliyotajwa katika mkataba zimerudisha majibu kwamba hazifahami lolote kuhusu majina ya wawakilishi waliotia saini mikataba na Benki Kuu isiyoeleweka. Simu zimepigwa moja kwa moja Valmet (hivi sasa Metso Paper) nchini Marekani, Mirrlees Blackstone (hivi sasa Man B&W Diesel Limited) ya Uingereza na Daimler Benz AG (hivi sasa Daimler Chrysler) huko Marekani na majibu yakarudi kwamba wahusika wakuu hawajui lolote kuhusu mikataba na Benki Kuu ya Tanzania.

Barua kwa Gavana Ballali, kutoka kwa Samuel Sithole wa Deloitte & Touche nchini Afrika Kusini inasema wazi kwamba “matumizi ya majina ya zamani ya kampuni na kasi ya ufanikishaji wa makubaliano na mikataba inathibitisha wazi kuwepo kwa ufisadi uliohusu maofisa waandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania.”

Kampuni ya Deloitte & Touche ilielezea pia mashaka yake kuhusu jinsi kampuni ya Kagoda, ilivyoundwa Septemba 29, 2005, na kuweza kulipwa “dola milioni 30.8 katika kipindi cha wiki tano hadi sita tu ya kuundwa kwake.”

“Hatuna taarifa zozote kuhusu uchunguzi wowote uliofanywa na Benki kuu kuhusu kampuni hiyo. Ni vigumu pia kukubali kuwa kampuni hizo ziliweza kuingia mkataba wa malipo ya dola milioni 30 na wadai mbalimbali nchini Ujerumani, Italia, Yugoslavia, Uingereza, Ufaransa, Marekani na Japan kwa kipindi kifupi,” inasema sehemu ya waraka huo.

Wakaguzi hao wa hesabu walimshauri Dk. Ballali kufanya ukaguzi wa haraka na wa kina na kusimamisha ajira za maofisa kadhaa wakati wa uchunguzi kuepuka kuharibiwa ushahidi wa nyaraka katika mafaili muhimu.

Hata hivyo hadi leo hakuna ofisa wa Benki Kuu aliyesimamishwa ajira yake hadi sasa kuhusiana na suala hilo. Hivi sasa kampuni mpya ya Massawe Ernst & Young, imepewa zabuni kukagua upya hesabu za kihasibu ndani ya Benki Kuu kwa mwaka 2005/06.

Hata hivyo taarifa za uchunguzi mpya bado ni siri ya Serikali licha ya taarifa za wazi kwamba umekamilika.

Hata mtu wa pili, hajulikani anakokwenda. 25 Juni 2006 alilizungumzia suala hili Bungeni na kutaka kupata ufafanuzi.
Katika taarifa ACG ya mwaka 2005-2006 Tanzania imenyimwa fedha kwa sababu wafanyabiashara wakubwa wamechota na hawajarudisha.

Mmmoja wapo aliyetajwa katika ripoti ya ACG, ni Rostam Aziz.

No comments: