Saturday, January 26, 2008

Hawa ndio wenyewe?


WATU watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma za kuvamia ofisi za gazeti la MwanaHALISIi na kummwagia kemilikali inayodhaniwa kuwa tindikali Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo Saed Kubenea na kumjeruhi kwa sime Mshauri wa gazeti hilo, Ndimara Tegambwage.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Polisi, Charles Kenyela aliwataja washtakiwa hao mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Addy Lyamuya kuwa ni Alex Mwandemele (28) maarufu kwa jina la Chusa mkazi wa Kigogo na Hashim Mndoe (32) maarufu kwa jina la Madilu wa Tegeta.
Wengine ni Augustino Joseph (30) maarufu kwa jina la Cheusi wa Mwananyamala, Hamis Ramadhani (25) wa Mwananyamala na mkazi wa Kinondoni Alfred Moshi (64), maarufu kwa jina Chambya.Kenyela alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na makosa ya kula njama ya kujeruhi, kummwagia tindikali Kubenea na kumjeruhi Ndimara Tegambwage.

No comments: