Tuesday, December 16, 2008

Mgonja afikishwa mahakamani
KATIBU mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha nchini, Gray Mgonja amefikishwa mahakamani mjini Dar es Salaa na kusomewa mashitaka tisa ya matumizi mabaya ya madaraka. Mgonja ni miongoni mwa viongozi 11 walotajwa na wabunge wa upinzani Agosti 2008.
Mbali na Mgonja wengine waliotajwa ni Rais Jakaya Kikwete na rais mstaafu Benjamin Mkapa ambao wapinzani wametaja kuwa wamefilisi nchi kwa kile kilichoitwa “vitendo vya ufisadi.”“Ama wameruhusu, au wameidhinisha, au wamenyamazia, ufujaji wa mamilioni ya fedha za umma,” viongozi wa upinzani wameeleza jijini Dar es Salaam.
Pamoja na Kikwete na Mkapa, ni Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Gavana wa Benki Kuu (BoT) Daudi Balali, mawaziri Basil Mramba, Andrew Chenge na Nazir Karamagi.Wengine ni Mweka Hazina wa CCM, Rostam Aziz, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Patrick Rutabanzibwa na Wakili maarufu Nimrod Mkono ambaye sasa ni mbunge wa Musoma Vijijini.
Je, hiyo ni dalili kwamba serikali imedhaniria kupambana na ufisadi? Au kuna watu wanatazamwa na wengine hawataguswa? Je, wanamtandao kama Lowassa na Rostam watafikishwa mahakamani? Ngoja tuone.

No comments: