Friday, March 14, 2008

Tunakwenda Comoro kwa maslahi ya nani?Mawaziri wawili wa serikali ya Tanzania, Benard Membe naHussen Mwinyi, wametangaza vita dhidi ya kiongozi wa kisiwa cha Anjouan, Kanali Mohamed Bacar kwa kile wanachodai kwamba "kiongozi huyo yupo madarakani kinyume cha sheria. "Mawaziri hawa vipenzi vya Rais Jakaya Kikwete, wamewaambia waandishi wa habari leo (Ijumaa 14 Machi 2008), kwamba Tanzania ndiyo itakayoongoza katika vita ya kumuondoa madarakani Kanal Bacar.

Je, kwa utaratibu huu wa madkiteta wa AU (Umoja wa Afrika), kubeba shauku ya kutaka kung'oa katika madaraka kila kiongozi wasiyemtaka na hata kama amechaguliwa na wananchi wake na kuweka kibaraka wao, tutarajie nini huko mbele?
Je, iwapo ikitokea mtu akadai kwamba Jakaya Kikwete, si rais halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madai kwamba uchaguzi wa Zanzibar, moja ya sehemu muhimu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haukuwa huru na haki, atasemaje? Je, atakubali kung'olewa madarakani? Lakini mbona hatua hiyo haikuchukuliwa kwa Mwai Kibaki, ambaye dhahiri hakushinda uchaguzi.

Huku kama si kwenda kuwauwa ndugu zetu ni nini hasa?

2 comments:

Anonymous said...

hakuna kitu kibaya kama kutoona mbele na tabia ya kupenda kusifiwa, hii ni tabia ya nchi kama marekani yenye kudhani inauwezo wa kufanya watakalo kwa maslahi yao, sasa hoja ya sisi watanzania kwenda comoro bado haileti maana kwetu na wala haionyeshi kwamba tunatofauti na mwrekani iliyoivamia iraq kwa visingizio mbali mbali ,inawezekana tz kwa kutembelewa na bush labda inaamin na yenyewe ni taifa kubwa, labda tuendelee kuiuliza tz, ni nini maslahi yetu comoro ,maana marekani maslahi yake iraq ni mafuta na wanaendelea kuyachukua kwa nguvu zote huku wakiiacha nchi kuendelea kuwa masikini kwa kila hali na kupungua kwa amani kilasiku, au labda ndugu yetu huseni anaonyesha nguvu zake kwa mara ya kwanza kwamba nguvu ya nchi ni kuonea wanyonge, ila ni vyema wakaelewa, tz haijawahi kuwa na maadui wa kisiasa hasa nje ya nchi na huu ni mwanzo mbaya kwa uongozi wa huseni, angalia rumsfeld alisema uongo na mwisho ulimshinda kuuthibitisha na hatimae aliachia uongozi. jee ndugu yetu unliona hilo, jee wa tz unatak tuwe na sura ya wamarekani nje ya nchi au tupe somo ni lini tz imekuwa mtawala wa afrika na kwamba ndio nchi ya kupigiwa mfano ,angalia wazee wanasema usipewe pima ukachukua nyanda, sisi vijana wenzako tupo na tunakuangalia, kupewa dhamana sio kwamba eti wewe ndiye mjuzi na hivyo unaweza kufanya utakalo. kumbuka cheo ni dhamana na dhamana kubwa uliyopewa ni kulinda heshima yetu wa tz nje na ndani ya nchi angalia mno hatupendi picha yetu ya nje ituweke kama wamarekani wawapo nje ya nchi, kumbuka kila jeshi letu liwapo nje ya nchi lazima lipate maoni na matakwa ya wananchi kwa faida wyao sio yako wewe na kwa faida yako.