Sunday, March 16, 2008

Padri Mlawiti bado ang'ang'aniwa

Kanisa Katoliki nchini, limesema litamshitaki upya Padri Sixtus Kimaro ambaye juzi alichiwa huru na Mahakama Kuu ya Tanzania, baada ya kushinda rufaa yake iliyopinga adhabu ya kifungo cha miaka 30 aliyopewa na Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu Dar es Salaam.

Padri Kimaro alipatikana na hatia ya kulawiti na shambulio la aibu. Alitakiwa pia kumlipa kijana aliyemshambulia Sh 2milioni.

Askafu Mkuu Msaidzi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Dk. Methodius Kilaini, amesema Kanisa hilo lina mahakama yake na kwamba litamfikisha Padri Kimalo ili kujiridisha kwamba bado anayo hadhi ya kukabidhiwa kuchunga kondoo wa bwana.

No comments: